Thursday, 12 July 2018
Friday, 22 June 2018
Na George Mganga
Imeelezwa kuwa Mshambuliaji mpya wa Yanga kutoka Benin, Marcelin Koukpo tayari amefanyiwa vipimo vya afya na sasa yu tayari kuanza mazoezi na kikosi kuanzia wiki ijayo.
Taarifa zinaeleza kuwa Koukpo tayari alishawasili nchini muda mrefu na panapo majaaliwa wiki ijayo ataungana na wachezaji wenzake kuanza kujifua kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.
Daktari wa Yanga, Edward Bavu amekamilisha kumfanyia vipimo hivyo Koukpo ambaye alikuwa anaichezea Les Buffles ya nchini kwao kabla kujiunga na Yanga na kuonekana yupo fiti kiafya.
Koukpo tayari ameshamalizana na mabosi wa Yanga kupitia Mwenyekiti wa usajili, Hussein Nyika kwa kusaini mkataba wa miaka miwili.
Baada ya kukamilisha vipimo kwa mchezaji huyo, inaelezwa kuwa Yanga ipo kwenye mazungumzo na wachezaji wengine ikiwemo Mohamed Ibrahim wa Simba ambaye alikosekana katika michezo mingi ya msimu uliomalizika

Monday, 11 June 2018
“ tumesikia wachezaji baadhi tu ndio wana mikataba na klabu kwa sasa wengi mikataba yao imekwisha. Jukumu la kamati yetu kwanza kabisa ni kurudisha heshima ya Yanga nchini pia kuifanya timu ya ushindani kimataifa. Tutakutana haraka kuona nini kifanyike ili kuipa nguvu timu. Nguvu ya timu ni ubora wa wachezaji na bechi la ufundi kwa matokeo chanya. Si kazi ndogo lakini tutahakikisha tunafanya kile tunachoweza kwa dhamana tuliyopewa na wanachama na Mungu atasaidia. Kikubwani ushirikiano pande zote kwa masilahi mapana ya klabu.‘
- Tarimba Abbas

Sunday, 10 June 2018

Kiungo Papy Tshishimbi ameondoka nchini na kurejea kwao DR Congo kwa ajili ya mapumziko.
Tshishimbi amekuwa akihusishwa na kujiunga na Simba, jambo ambalo limewapa hofu na hasira baadhi ya mashabiki wa Yanga.
Tshishimbi hakuwa amewahi kulizungumzia suala hilo lakini jana amekutana na Salejembe jijini Nairobi, Kenya na kuweka wazi kila kitu.
Tshishimbi amesema anareja kwao kwa mapumziko akiwa bado ni mchezaji wa Yanga na atarejea baada ya mapumziko.
Kuhusiana na suala la Simba, hii ndiyo kauli yake.
“Kuhusu Simba ninasikia tu kwa kweli. Lakini hakuna ambaye amewahi kunifuata tukalizungumzia suala hilo.”
Alipoulizwa kama Simba wakimfuata, yuko tayari kujiunga nao?
“Soka ni biashara rafiki yangu, unajituma na kufanya vizuri ili upae kibiashara na kujiendeleza zaidi. Timu ikifanikiwa, soko linakuwa juu.
“Kama Simba wananihitaji, niko tayari wanaweza kusema wanahitaji nini nami niangalie.”

Saturday, 9 June 2018
Kuelekea Mkutano Mkuu wa Yanga unaofanyika Jumapili ya leo katika ukumbi wa Police Officers Mess jijini Dar es Salaam, Katibu wa Baraza la Wazee wa klabu hiyo, Ibrahim Akilimali ametoa neno lake.
Mzee huyo ambaye awali alionekana kupinga mabadiliko hayo amesema kuwa kwa sasa anayaunga mkono kwa asilimia zote.
Akilimali ameeleza kuwa mabadiliko Yanga kwa sasa hayakwepeki kutokana na timu yao ilipofikia hivi sasa mpaka kwa mwenendo ilionao kuwa si mzuri.
Kiongozi huyo amesema yeye hajawahi kupinga mabadiliko bali alikataa mfumo ambao alikuja nao Yusuph Manji hapo awali akitaka kukodisha timu na nembo jambo ambalo amefunguka kwa kueleza halikuwa sahihi kwake hata kidogo.
Ikumbukwe wakati Manji akiwa Mwenyekiti Yanga, alikuja na ombi la kutaka Yanga aikodishe akihitaji timu na nembo na baadhi ya wanachama ikiwemo Akilimali na wengine kuibuka na kupinga kwa nguvu suala hilo.
Mkutanoo Mkuu wa Yanga unatarajia kuanza leo majira ya saa 4 kamili za asubuhi ambapo Waziri mwenye dhamana ya michezo, Harrison Mkwayembe anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

Baada ya Simba kumtimua Kocha Mkuu, Mfaransa, Pierre Lechantre, mabosi wa timu hiyo wamefikia uamuzi wa kuikabidhi timu hiyo kwa Mrundi, Masoud Djuma Irambona ambaye atasaidiwa na mkongwe, Selemani Matola.
Djuma ambaye ndiye kocha msaidizi wa Simba kwa sasa, yupo na kikosi hicho mjini hapa Nakuru ambapo Simba inajiandaa kucheza mchezo wa fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup dhidi ya Gor Mahia, kesho Jumapili.
Alhamisi ya wiki hii, mabosi wa Simba walimpiga chini Mfaransa huyo baada ya kushinikiza kupewa mkataba mpya licha ya kuambiwa asubiri mpaka timu itakaporudi Dar.
Lechantre alitofautiana na vigogo wa Simba baada ya kushinikiza mabadiliko makubwa kwenye mkataba wake ikiwemo mshahara wa Sh 90milioni kwa mwezi pamoja na kupandishiwa posho zote na hata ndege asafiri kwenye daraja la kwanza.
Kwa mujiv=bu wa gazeti la Championi limedokezwa na kiongozi mkubwa wa Simba kwamba baada ya timu hiyo kuwasili jijini Dar ikitokea Kenya, Djuma atatangazwa kama kocha mkuu huku msaidizi wake akiwa Matola ambaye msimu uliopita alikuwa kocha msaidizi wa Lipuli ya Iringa.
Matola ndiye nahodha wa mwisho kuipeleka Simba kwenye robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2003.
“Tumeamua kumuongeza Matola kwenye kikosi chetu kwa kuw atuna imani naye hivyo atakuwa msaidizi chini ya Djuma, tumepanga kumtambulisha mara tu tutakaporejea Tanzania.
“Kwa sasa tumeamua kufanya hivyo kwani tumeona ni bora kuwatumia makocha wa Kiafrika zaidi hasa wa ukanda wetu huu ambao wanajua vizuri staili ya soka letu kuliko Wazungu,” kilisema chanzo.
Alipotafutwa Matola alisema: “Bado sijapata taarifa kuhusiana na hilo lakini tungoje kwanza nitaweka wazi baadaye.”
Hakuna kiongozi wa Simba aliyekuwa tayari kuzungumzia ishu hiyo jana kwa kutajwa jina, huku wengi wakidai watatoa ufafanuzi baadaye.
