Friday, 18 May 2018

Yanga yamalizana watatu kuipa nguvu kwenye kombe la shirikisho

Na George Mganga Uongozi wa klabu ya Yanga kupitia kwa Katibu wake, Charles Boniface Mkwasa, umesema yauari umeshamalizana na wachezaji watatu watakaokuwa na timu hiyo. Mkwasa ameeleza kuwa watawataja wachezaji hao siku za hivi karibuni ambao watakuwa mhimili mkubwa katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika. Yanga ilipewa nafasi tatu na CAF kusajili wachezaji ili kukipa nguvu kikosi chao ambapo kipo kwenye mashindano hayo ya kimataifa. Mkwasa amesema hataweza kuwaweka wazi wachezaji akidai wanaweza wakapokonywa na baadhi ya klabu za hapa nchini hivyo wakati ukifika utawataja. Juzi Jumatano Yanga imekwenda sare na Rayon Sports ya Rwanda ikiwa ni mchezo wa pili wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho. Wakati huo timu hiyo ipo njiani hivi sasa kuelekea Shinyanga kwa ajili ya mechi ya ligi dhidi ya Mwadui FC itakayopigwa Uwanja wa CCM Kambarage. Kutoka Spoti Leo - Radio One

0 coment�rios: