Mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara na mabingwa wa kombe la FA Simba Sc wanatarajia kutest mitambo yao tena weekend hii kabla hawajakatana jumatano hii,wekundu wa msimbazi wao walioweka kambi yao unguja watamenyana na Gulioni Fc jumamosi ya leo saa 1:30 jioni,huku watoto wa jangwani wao wakitest mitambo yao siku ya jumapili hii wakiumana na Jamhuri ya Pemba,macho na masikio katika michezo hiyo yanatarajiwa kuelekezwa uwanja wa Gombani ambako ndilo litakakopigwa pambano la Yanga Africans na Jamhuri kikubwa ikiwa ni kiungo mcongomani Papy Kabamba Tshishimbi aliyetua ijumaa hii kambini huko kama atapewa nafasi ya yeye nae kutest mitambo yake,Tshishimbi amekuwa gumzo kutokana na usajili wake kuwa masikioni mwa wapenda soka Tanzania kwa muda sasa.
0 coment�rios: