Saturday, 19 August 2017

Tukio kuɓwa kutokea August 21

Jumatatu ya tarehe 21 Agosti, tukio lisilo la kawaida litashuhudiwa Amerika Kaskazini. Kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1918, jua litapatwa kikamilifu na mwezi Marekani. Bara lote la Amerika Kaskazini litafunikwa na giza totoro mchana. Ingawa baadhi ya watu wanalitazama tu kama tukio la kuvutia, kwa wengine linaashiria mwisho wa dunia. Mfano makundi mbalimbali ya kidini nchini Marekani yameanza kuhubiri kwamba tukio hilo linaashiria kukaribia kwa mwisho wa dunia. (BBC)

Toa maoni yako

0 coment�rios: