SI KILA SHIDA YA MWANAMKE HUTATULIWA KWA PESA TU, JIFUNZE KUJALI ANAYOPITIA!
Si kila wakati mwanamke anapokuambia anashida basi anatafuta pesa tu, si kila wakati mwanamke akiwa na shida kweli ni lazima umpe msaada wa kifedha. Matatizo mengi ya wanawake yanahitaji kusikilizwa kwanza, mpenzi wako au mke wako anataka mtu wa kumsikiliza, mtu wa kumuambia matatizo yake na kumpa moyo. Hakuna kiasi chochote cha pesa ambacho kinaweza kutatua matatizo yake.
Kitu ambacho sisi wanaume tunasahau nikuwa mwanamke hata yeye anaweza kutafuta pesa lakini kamwe hawezi kujisikiliza. Wanaume wengi ambao wanajiona wanahonga, wanajiona wana hela nyingi huishi kutoa pesa tu, anakuambia anataka kuongea na wewe unamuuliza unataka shilingi ngapi, unadgani kuwa pesa zitatatua kila kitu, unadhani wewe ni mwanaume bora kwa kutoa pesa tu!
Nikweli wakati mwingine anataka hela, ana tatizo lakini anataka umsikilize, akuambie tatizo lake, alie ndiyo kama kuna haja ishu ya hela basi akuambie. Tuchukulie kwa mfano, mke/mpenzi wako anauguliwa na Mama yake, nikweli pesa zitasiadia sana, lakini anataka bega la kulilia, akuambie namna ambavyo anajisikia, namna ambavyo anaumia Mama yake anaumwa.
Anataka mtu wa kumuambia usiwe na wasiwai atapona, mtu wa kuhangaika naye kutafuta watu wa kumuongezea damu, mtu wa kuwa naye wakati madaktari wanamuambia Mama yake anahitaji upasuaji. Unatakiwa kujua kuwa mbali na kuwa mpenzi wake wewe ni rafiki yake, si jirani yake ambaye utamkopesha pesa tu, hembu kua mpenzi na jifunze kuwa bega lake wakati analia, msikilize!
0 coment�rios: