ulimwengu wa soka Tz
Sergio Aguero ameshafanyiwa vipimo baada ya taarifa kwamba alikuwa anajisikia kuumwa baada ya mechi ya kichapo cha 4-2 kutoka kwa Nigeria mechi ya kirafiki jijini Krasnodar.
Straika huyo wa Manchester City alianguka wakati wa mapumziko na haraka sana akapelekwa katika Hospitali ya karibu kabisa na ulipo uwanja na baadae aliruhusiwa na kujiunga na kikosi cha Argentina.
Taarifa kutoka Shirikisho la soka la Argentina kupitia ukurasa wao wa Twitter inasema," Aguero alizimia na alipelekwa Hospitalini kwa uchunguzi zaidi ambao ulifanyika kama tahadhari."
Akirejea kuhusu tatizo lake la zamani la Moyo daktari watimu ya taifa ya Argentina Dokta Donato Villani amewaambia waandishi wa Habari ," alijisikia vibaya mara mbili , na historia yake ya kitabibu ambayo anayo tangu alipofanyiwa operesheni akiwa na umri wa miaka 15 tulitaka kuwa na uhakika kwamba hakuna kitu kibaya zaidi."
" Tulimpeleka Hospitali kuhakikisha kwamba kila kitu kipo kawaida , tunapenda kusubiria ili tuwe na uhakika zaidi."

0 coment�rios: