Habari kutoka azam fc
Mchezaji kinda wa Timu ya soka ya Azam FC Shaban Idd Chilunda atarejea uwanjani katika michuano ya Mapinduzi ambayo inaanza Disemba 30 mwaka huu baada ya kukaa nje kwa takribani miezi minne akiuguza majeraha.
Akiithibitishia Futaa.co.tz afisa habari wa Azam FC Jaffary Idd Maganga amesema kuwa amewasiliana na Daktari mkuu wa timu, Dokta Mwanandi Mwankemwa ambaye amemtaarifu kuwa Chilunda yupo fit na anaweza kuanza kucheza hivyo basi watamjumuisha kwenye kikosi kitakachokwenda Zanzibar.
-Mchezaji Shaban Idd Chilunda ambaye muda mrefu hajaonekana uwanjani toka kuanza kwa ligi tunatarajia katika mashindano ya Mapinduzi cup, kwa mujibu wa daktari wetu, ataanza rasmi kurejea uwanjani lakini hatoweza kujumuika for full, atapewa at list dakika 20 ama 30 kumuweka sawa,” Amesema Maganga.
Shaban alipata mataatizo hayo akiwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’ wakati ikishiriki michuano ya Kombe la baraza la vyama ukanda wa Afrika ya Kusini ‘COSAFA’ iliyofanyika katikati ya mwaka huu.
Mchezaji bora
Ikumbukwe kuwa tuzo ya mchezaji bora kijana (U20) ambayo imepewa jina la Ismail Khalfani Mrisho aliyekuwa mchezaji wa Mbao ambaye alifariki uwanjani akiitumikia timu yake kwenye mashindano ya ligi ya vijana, ilichukuliwa na Shabani Idd Chilunda wa Azam FC ambaye katika mashindano hayo alifunga mabao 7.
Aidha katika michuano ya mapinduzi Azam ambao ndio mabingwa watetezi imepangwa Kundi A, pamoja na timu za Simba SC ya Jijini Dar es Salaam, Jamhuri SC na Mwenge SC zote za Zanzibar, pamoja na URA ya Uganda.
Tanzania Azam FC Mapinduzi Cup Jaffary Iddi Maganga/Tanzania Shaban Idd Chilunda (Tanzania) COSAFA Cup 2017 Credit #futaacom
0 coment�rios: