Msikie Masau Bwire Msemaji wa Ruvu shooting
“Tunakwenda kucheza na mabingwa tunawaheshimu sana ni timu ambayo ina mashabiki wengi wanaoiunga mkono, timu ambayo ipo kwenye mpira kwa muda mrefu kuliko Ruvu Shooting lakini hiyo haitoshi kusema kwamba kwa sababu wao ni mabingwa basi watatufunga.
.
“Tumejipanga kwa mapambano tena yatakuwa mapambano makubwa na watanzania watakapohitaji kuona mpira ambao umejitosheleza kiufundi, umahiri, uhodari, wangalie mchezo wa Ruvu Shooting dhidi ya Yanga.” - Masau Bwire, msemaji wa Ruvu Shooting akiongelea mchezo wa leo vs Yanga!

0 coment�rios: