Sanchez safarini , Manchester.
Alexis Sanchez aliikosa mechi ya ushindi ya Arsenal (4-1) dhidi ya Crystal Palace hapo jana kwasababu alikuwa anasafiri kuelekea kaskazini kwenda kuzungumza kuhusu uhamisho wake wa kutua Manchester United, amesema Arsene Wenger.
"Sikumjumuisha kikosini kwasababu kulikuwa na swala la yeye kuhamia Manchester United na huwezi kuendesha gari kwenda Kaskazini na pia ucheze mechi."
"Hiyo ni ngumu ndio maana niliamua kumuacha kikosini"
" Natarajia uhamisho kukamilika lakini siwezi kutangaza kwasababu katika saa 48 zijazo utaamuliwa kwa njia moja au nyingine."
"Kwa vitu kama hivi kama bado havijakamilika huwezi kusema kwamba itakamilika kwasababu mazungumzo ya makubaliano huwa yanachukua muda mrefu hiyo ni kwasababu siku hizi kila taarifa ni muhimu sana"
"Kama unataka kubashiri, basi bashiri kwamba uhamisho utafanyika."Credit #Ulimwengu wa soka Tz
0 coment�rios: