Friday, 23 February 2018

Conte yupo tayari kusitisha vita.

Antonio Conte ameonyesha nia ya kutaka kumaliza vita ya maneno dhidi ya Jose Mourinho kuelekea mechi baina ya vilabu vya Manchester United dhidi ya Chelsea. Makocha hao wawili wanatarajiwa kukabiliana kwenye mtanange wa siku ya Jumapili katika dimba la Old Trafford na Conte anafikiria kuhusu mechi tu . Conte na Mourinho wamekwaruzana mara kadhaa katika msimu huu , wakitupiana maneno makali katika muendelezo wa ugomvi wao hadharani. Kuelekea mechi hiyo ya kuwania nafasi nne za juu katika ligi kuu ya soka ya Uingereza , Conte anaamini kwamba muda umefika sasa wa kuchora mstari kuhusu jambo hilo na kusonga mbele. " Siitaki tena hii mada. Wote tumesema vitu hapo nyuma, lakini tumalize. " Amesema Conte. " Kwangu mimi, hii hali lazima isitishwe." Kama Conte, Mourinho naye yupo tayari kumaliza hii vita na kuzingatia maswala ya soka tu na kuweka ugomvi binafsi pembeni. " Nilishawaambia hapo awali sitaki kuzungumza kuhusu hilo. Sitaki kabisa." Mourinho aliwaambia waandishi wa habari siku ya Ijumaa. " Hiyo sio pointi. Ni kocha mzuri, timu nzuri na hilo ndio muhimu kwangu . hilo tu."Credit #UlimwenguwasokaTz

0 coment�rios: