Tuesday, 27 February 2018

Mechi ya Mtibwa sugar vs Yanga imepigwa kalenda

Bodi ya ligi kuu Soka Tanzania bara (TPLB) imeahirisha mchezo wa ligi kuu Soka Tanzania bara Kati ya Mtibwa Sugar dhidi ya Mabingwa watetezi Yanga. Mchezo huo uliopangwa kuchezwa katika dimba la Jamhuri Mjini Morogoro Tarehe 3 ya mwezi Ujao sasa utapangiwa siku nyingine ili kutoa fursa Kwa Yanga ambao ni wawakilishi wa Tanzania bara kwenye michuano ya klabu bingwa barani Afrika kujiandaa na mchezo wao wa raundi ya kwanza ya Township Rollers ya Botswana mchezo utakaochezwa Tarehe 6 Machi hapa Dar es Salaam. Awali Yanga walipeleka ombi la kusogezwa mbele Kwa mchezo huo na Bodi ya ligi wakapitia na kuamua kukubali maombi ya Yanga. Kesho Yanga itakua katika dimba la Nangwanda Mjini Mtwara kucheza dhidi ya Ndanda FC ya huko kabla ya kurejea jijini Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wake wa kimataifa.

0 coment�rios: