Sunday, 18 March 2018

Haji Manara: Sasa tutawaonyesha

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Klabu ya Simba SC, Haji Manara amefunguka na kusema kuwa hivi sasa Simba na mashabiki wa Simba hawawezi kuwa wazalendo kwa Yanga bali uzalendo pekee watakuwa nao kwenye timu ya taifa tu. Haji Manara amesema hayo siku moja baada ya Simba kuondolewa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho huku Yanga nayo ikiwa imeondolewa katika michuano ya Klabu Bingwa Barani Afrika. Baada ya timu hizo kuondolewa kwenye michuano hiyo zote zikiwa ugenini na kutoka kwa suluhu ya bila kufungani mashabiki wengi walianza kutoa lawama kuwa timu hizo ni kwa kuwa zilishindwa kujipanga vyema na kutumia vizuri uwanja wa nyumbani. "Naona huko mitandaoni baadhi ya wanayanga wanataja sababu mojawapo ya timu za bongo kutofanya vizuri uwanja wa nyumbani ni kukosa uzalendo kwa vilabu vyetu....wanalosahau wao nililisema hadharani mapema na nikabezwa na viongozi wao..leo ndio mwaujua uzalendo? Nawaambia kwa sasa tutafanya zaid yenu..kama tudini tudani....uzalendo wetu utabaki kwa timu za Taifa tu" alisisitiza Haji Manara.

0 coment�rios: