Saturday, 17 March 2018

Kaimu rais wa Simba mr Try again amesisitiza watapambana mpaka tone la mwisho

Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ amesema watapigana hadi tone la mwisho kuhakikisha wanashinda leo dhidi ya Al Masry. Akizungumza mjini hapa, Try Again amesema wamekuwa wakijitahidi kufanya kila kitu kinakwenda kwa usahihi. “Tunapambana sana, umeona nami nimesafiri na timu hadi huku. Viongozi wote tuko hapa, tunakula pamoja, tunaishi pamoja na hii ni kuonyesha tuko pamoja na tunataka jambo moja. “Tunaendelea kuwa makini lakini mapigano yetu ni hadi mwisho tutakapopata tunachotaka dhidi ya Al Masry,” alisema. Rais huyo kwa kushirikiana na viongozi wa kamati ya utendaji wamekuwa karibu kuhakikisha kila jambo linakwenda sahihi kabla ya mechi ya leo. Simba ipo hapa Port Said kwa ajili ya mechi ya pili ya Kombe la Shirikisho dhidi Al Masry.

0 coment�rios: