Kisa fedha za CAF wachezaji wa Yanga waapa kufia uwanjani leo
Kama Yanga kifuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika itapata Sh bilioni 1.1, sasa wachezaji wake wameapa kufia uwanjani ili waifunge Township Rollers FC katika mechi yao ya leo Jumamosi.
Rollers inaivaa Yanga leo katika mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye Uwanja wa Taifa uliopo Gaborone, Botswana ambapo awali ilishinda mabao 2-1 ugenini jijini Dar es Salaam.
Ili isonge mbele hatua ya makundi, Yanga inabidi ishinde kwa uwiano wa mabao 2-0, lakini hata ikitolewa itatupwa katika hatua ya kufuzu makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Wachezaji wa Yanga wakiongozwa na mshambuliaji Ibrahim Ajibu wameapa kupambana kufa na kupona ili waweze kutinga hatua ya makundi na kupata Sh bilioni 1.1 kutoka Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ambao ni waandaaji wa michuano hiyo.
Akizungumzia mchezo huo kutoka Gaborone, Ajibu alisema; “Tumejipanga kuhakikisha tunaibuka na ushindi na hatutakubali kufungwa kirahisi kama ilivyokuwa katika mechi yetu ya kwanza, hakika tutafia uwanjani kesho (leo).”
0 coment�rios: