Thursday, 8 March 2018

Rostand: Bado tuna nafasi kubwa

Klabu ya Yanga SC imeshindwa kutamba katika Uwanja wake wa Nyumbani baada ya kukubali kipigo cha Magoli Mawili kwa moja dhidi ya wapinzani wao kutoka Botswana Township Rollers. Licha ya kufungwa huko Lakini kipa wa timu hiyo Youthe Rostand Amesema kuwa Bado wana nafasi kubwa kuingia katika hatua ya makundi ya Klabu Bingwa Afrika. "Malengo yetu ni kuingia katika hatua ya makundi ya Klabu Bingwa Afrika msimu Huu,tumepoteza mchezo wa nyumbani na hii sio Mwisho na haitukatishi tamaa,bado tuna nafasi kwani bado kuna Mchezo wa marejeano tutatumia mda huu kufanya mazoezi na kwenda kufanya vizuri". Amesema Rostand. Yanga itacheza Mchezo wa marejeano huko mjini Gaborone,Botswana ikienda kutafuta Ushindi ili kuingia katika makundi ya Klabu Bingwa Afrika na Ikishindwa itaangukia Katika kombe la Shirikisho Afrika.

0 coment�rios: