Singida utd imewashindwa vigogo
Singida United imeshindwa kutamba mbele ya vilabu vikubwa baafa ya kukubali kichapo cha bao 1-0 mbele ya Azam kwenye mchezo wa ligi uliochezwa uwanja wa Azam Complex usiku wa leo.
Singida ilishindwa kupata ushindi wakiwa uwanja wa nyumbani dhidi ya Yanga na kulazimishwa sare ya bila kufungana.
Wakapoteza 4-0 mbele ya Simba uwanja wa taifa, wameambulia pointi mbili dhidi ya vigogo (Singida Unite 1-1 Azam, Singida United 0-0 Yanga, Simba 4-0 Singida United, Azam 1-0 Singida United).
Azam imefikisha pointi 38 kwenye msimamo wa ligi pointi mbili nyuma ya Yanga ambayo inamchezo mmoja mkononi huku Singida wakibaki katika nafasi ya nne wakiwa na pointi 34.
Nguvu na kasi ya Singida United inazidi kupungua, wakati msimu unaanza ni tofauti na sasa. Changamoto kama hizo wakati mwingine hutokea lakini ni jinsi gani mwalimu Hans ataweza kuhakikisha wachezaji wanarejea katika mstari wao ili timu iendelee kupata matokeo.
Kuna baadhi ya mechi walikuwa wanakosa wachezaji wao muhimu lakini bado wana kikosi cha kupata matoke.
Lakini tukumbuke hii ni raundi ya pili kila timu inahitaji matokeo ili kutimiza malengo yake, zipo timu ambazo zinahitaji ubingwa lakini kuna timu ambazo zinataka kubaki kwenye ligi.
0 coment�rios: