Tuesday, 17 April 2018

Kambale ametaja maana ya jina lake “Tanzania mnafikiri ni samaki”

Jina la mshambuliaji wa Singida United Papy Kambale limepata umaarufu haraka nchini kutokana na maana ya jina hilo hapa Tanzania. Ukitaja ‘Kambale’ moja kwa moja vichwani mwa watanzania inakuja picha ya samaki, maeneo mengi ya mikoa ya Tanzania wanaelewa Kambale ni aina ya samaki anaepatikana kwenye maji baridi (mtoni, bwawani, na kwenye maziwa yenye maji baridi). Kwa hiyo ndiyo maana jina Papy Kambale limekuwa maarufu sana kutokana na maana hiyo. Kumbe kwa kabila la mchezaji huyo jina Kambale lina maana nyingine kabisa na Kambale ameeleza maana halisi ya jina lake na kama kuna uhusiano wa jina lake la Papy na Papy Tshishimbi wa Yanga. “Jina la Papy ni maarufu sana Rwanda, jina languhalisi ni Kambale Salita lakini la Papy sio jina ambalo nilipewa na wazazi wangu ni kama A.K.A tu.” “Kwenye kabila letu Kambale ni jina la mtoto wa kwanza wa kiume ambaye anamfuata mwanamke lakini huku Tanzania mnafikiri ni samaki lakini kwenye kabila letu lina maana yake.” Kabla ya kujiunga na Singida United, Kambale alikuwa anacheza Rwanda lakini alikuwa anatamani siku moja acheze ligi ya Tanzania. “Nikiwa Rwanda nimecheza timu nyingi sana, nimecheza timu nne ikiwemo Rayon Sports na Kiyovu. Nilikuwa natamani sana kuja kucheza ligi ya Tanzania, mchezaji anakuwa yupo tayari kwa ajili ya timu yoyote inayomhitaji.” “Ligi ya Tanzania ni ngumu lakini ugumu wake unatusaidia uzoefu wa kucheza ligi nyingine ngumu kuliko ligi hii ya Tanzania.”

0 coment�rios: