Tuesday, 17 April 2018

Nsajingwa afungukia wasiwasi wao

Kocha Msaidizi wa Klabu ya Mabingwa Watetezi Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga, Shadrack Nsajigwa amedai timu yake itachukua tahadhari kubwa katika kupambana na wapinzani wao Welayta Dicha ili wasiweze kupata nafasi ya kushambuliwa lango lao, kwa lengo la kutaka kupata ushindi kwenye mechi hiyo Nsajigwa amebainisha hayo ikiwa yamebakia masaa machache kuelekea mtanange huo wa marudiano wa mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, utakaopigwa katika dimba la Hawassa mjini Hawassa nchini Ethiopia ambapo Yanga itakuwa na jukumu la kulinda ushindi wake wa 2-0 ilioupata kwenye mchezo wa kwanza uliofanyika uwanja wa Taifa Jijini, Dar es Salaam ili kuweza kujikatia tiketi ya moja kwa moja kuelekea katika hatua zinazofuata katika michuano hiyo. "Kimsingi nimshukuru Mungu mambo yote yanaenda vizuri pamoja na wachezaji wote tuliokuwa nao huku Ethiopia wapo salama kiafya. Mchezo wa leo utakuwa mgumu kama mnavyojua Welayta Dicha wanaweza kucheza mpira vizuri na wapo nyumbani, nafikiri watakuja kwa nguvu ili kusawazisha makosa yao waliyofanya katika mechi ya awali", amesema Nsajigwa. Pamoja na hayo, Nsajigwa ameendelea kwa kusema "sisi tumejiandaa vizuri katika kupambana nao nina amini kama Mwenyezi Mungu atatufikisha salama mpaka muda wa mchezo basi tutaweza kuiwakilisha vizuri nchi kwenye mechi yetu. Kwa kuwa wao wapo vizuri zaidi yetu hivyo tutachukua tahadhari za mapema kwa kulinda goli letu wasiwe kutushambulia huku sisi tukienda kwa kasi kwao kufanya mashambulizi ili tupate bao mapema". Kwa upande mwingine, Shadrack Nsajigwa amesema katika kikosi walichosafiri nacho mpaka sasa hakuna majeruhi yeyote ambaye atasababisha kukosa mtanange huo wa kukata na shoka

0 coment�rios: