Saturday, 28 April 2018

Vijana watakuwa na kazi ya kuwakabili Simba

Yanga inashuka dimbani kesho Jumapili ikiwa na vijana wanaopewa nafasi ya kuonesha upinzani mkali dhidi ya kikosi cha Simba kilicho kileleni mwa msimamo wa ligi. Vijana hao walionolewa na Kocha George Lwandamina, watakuwa chini ya Mkongomani, Mwinyi Zahera ambaye amekabidhiwa majukumu ya kukiongoza kikosi hicho huku akisaidiana na Noel Mwandila. Lwandamina alikitengeneza kikosi cha Yanga kwa kuwapa nafasi vijana ambao wamekuwa mhimili mkubwa ndani ya timu hiyo hivi sasa. Yusuph Mhilu, Pius Buswita, Emmanuel Martin, Abdallah Shaibu pia Rafael Daud wamekuwa sehemu ya kikosi cha kwanza na akiba kwa takribani msimu huu mzima tangu uanze. Wachezaji hao wanapewa nafasi kubwa ya kucheza katika mchezo dhidi ya watani wao wa jadi Simba, kesho Jumapili. Mechi hiyo yenye nguvu kubwa hapa nchini na ivutayo hisia kubwa kwa mashabiki wa soka, itafanyika Uwanja wa Taifa kuanzia saa 10 kamili jioni

0 coment�rios: