Wanachama wa Tandale waeleza kusalitiwa na Msajigwa
Baadhi ya wanachama wa tawi la klabu ya Yanga kwa Motogole, wameeleza kusikitishwa na Kocha Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa kutokana na kupoteza mchezo wa juzi dhidi ya Simba wakisema yeye ndiye chanzo.
Mmoja wa viongozi wakubwa ndani ya tawi hilo, amesema kuwa Nsajigwa amewasaliti akidai alitumika mpaka kusababisha Yanga ipoteze kwa bao 1-0 dhidi ya watani zao wa jadi, Simba.
Yanga ilifungwa mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa bao 1-0 na kujiwekea mazingira magumu ya kuendelea kuutetea ubingwa wa ligi.
Akizungumza kupitia Radio One jana jioni, Kiongozi huyo aliye na mamlaka makubwa ndani ya tawi hilo alieleza kuwa Nsajigwa alitumika kutengeneza matokeo huku akimtupia lawama akiuomba uongozi watafute mbadala wake akidai kuwa wakati wake umefikia mwisho.
Baada ya matokeo hayo, Yanga sasa imeweka nguvu zake zote kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya U.S.M Alger utakaopigwa Mei 7 huko Algeria.
0 coment�rios: