Friday, 4 May 2018

AKILIMALI:Serikali haitaki tuwe na Baba

Mjumbe wa Baraza la Wazee wa katika klabu ya Yanga, Mzee Ibrahim Akilimali, ameilalamikia serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa imewafanya kuwa yatima. Akilimali ameeleza kuwa serikali imesababisha Yanga kufikia mpaka hapo walipo huku akidai kuwa imewabana wasipate baba. Akizungumza kupitia Spoti Leo ya Radio One Stereo, Akilimali ameeleza kuwa Yanga hivi inapitia wakati mgumu kutokana na namna hali ilivyo mbaya klabuni. Mzee huyo ameigusia serikali kutokana na kuzuia mikutano kadhaa ya Yanga iliyopaswa kufanyika nyuma na mambo mengine huku akiilenga Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo iliyo chini ya Dkt. Harisson Mwakyembe. Kauli hiyo imekuja kufuatia baadhi ya nyota wa Yanga ikiwemo Obrey Chirwa, Papy Kabamba Tshishimbi na Ibrahim Ajibu kusalia nchini wakati kikosi kikisafiri kuelekea Algeria kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger utakaopigwa kesho.

0 coment�rios: