Uongozi Yanga wazungumzia kuhusu mechi ya leo na wachezaji ambao hawakusafiri na timu
Kuelekea mchezo wa leo wa Kombe la Shirikisho Afrika kati ya USM Alger dhidi ya Yanga, uongozi Yanga umesema wachezaji wake wako fiti kucheza.
Yanga itakuwa mgeni huko Algiers, Algeria katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya makundi unaotarajiwa kuanza majira ya saa 4 usiku leo.
Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, amesema kuwa wachezaji wote wako fiti na hakuna aliye majeruhi kuelekea mtanange huo.
Yanga imesafiri nchini Algeria ikiwa imewakosa nyota wake muhimu ikiwemo Kelvin Yondani, Ibrahim Ajibu, Papy Tshishimbi pamoja na Obrey Chirwa, ikielezwa kuwa wana matatizo mbalimbali.
Saleh Jembe Blog inawatakia kila la kheri Yanga kuelekea mchezo huo
0 coment�rios: