
Mkongo wa Yanga amesaini karandarasi ya miaka 2
Na George Mganga
Kocha Mkongomani wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu ya Yanga.
Zahera amechukua rasmi mikoba ya Mzambia aliyekuwa kocha mkuu wa kikosi cha Yanga baada ya kuondoka kimyakimya kurejea kwao Zambia katika klabu yake ya zamani, Zesco United.
Zahera alichelewa kusaini mkataba na Yanga kutokana na majadiliano baina yake na uongozi wa klabu hiyo, lakini sasa wamefikia mwafaka na ameamua kuweka kandarasi hiyo itakayomalizika mwaka 2020.
Awali kuna taarifa zilieleza kuwa Zahera amemtimkia kwao Congo kwa ajili ya majukumu ya kukitumikia kikosi cha timu ya Taifa ya Congo.

0 coment�rios: