
-Kocha mkuu wa Timu ya Yanga, Mwinyi Zahera ameanza harakati za usajili ndani ya klabu ya Yanga Sc kwa sasa amewaleta wachezaji 3 kwa ajili ya majaribio.
-Kwa sasa Mwinyi Zahera yupo kwao Congo amewaagiza wachezaji wawili kutoka kwao Congo kuja Yanga kufanya majaribio ni Mshambuliaji Alain Mulumba kutoka Motema Pemba na kiungo Cedrick Kabale kutoka Don Bosco. Wachezaji wote wawili wapo Dar na kesho jumatano wataanza mazoezi na timu hiyo.
-Pia Zahera amemleta mshambuliaji kutoka Nigeria, James Ugochukwu aliyekuwa anacheza soka la kulipwa Swaziland katika timu ya Manzini Wanderers na sasa tayari yupo Dar na jana alijiunga na klabu hiyo kwenye mazoezi yaliyofanyika katika uwanja wa Polisi Kurasini.
-Pamoja na kuleta wachezaji 3 kwenye mazoezi klabu ya Yanga kupitia kwa Kocha mkuu Mwinyi Zahera inafanya mpango wa kumleta golikipa wa timu ya Tp Mazembe, Ley Matampi ili kuchukua nafasi ya golikipa Mcameroon Youthe Rostand ambaye anadaiwa kutobadilika kila siku anafungwa magoli ya kizembe.
-Wachezaji wengine watatu wanachukua nafasi mbili za Mshambuliaji wa Zimbabwe Donald Ngoma ambaye amevunjiwa mkataba wake pia beki Mcongo, Festo Kayembe ambaye alisajiliwa na Yanga kwenye Dirisha dogo ila hajaonekana mpaka sasa.
-Yanga imepanga kwenda kwenye michuano ya Sportpesa Super Cup june 3-10 na wachezaji hao 4 kwa ajili ya kuwaangalia ikiwa watatu tayari wapo Dar huku Golikipa atakuja na kocha wa kikosi hicho Mwinyi Zahera mwisho wa mwezi huu.
yossima Sitta Jr.
0 coment�rios: