
Manji akubali kurejea lakini kwa sharti moja
Taarifa zinaeleza kuwa aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji, amekubali kurejea kurejea klabuni hapo endapo baadhi ya viongozi watakubali kuondoka.
Inalezwa Manji amekubali kiu ya wanachama na mashabiki wengi wa Yanga waliokuwa wakihitaji uwepo wake, haswa baada ya klabu yao kuyumba kiuchumi wakati akiwa amejiuzulu nafasi ya Uenyekiti.
Mapema leo bodi ya Wadhamini wa klabu hiyo chini ya George Mkuchika, ilikutana na Manji kwa ajili ya kumuomba aweze kurejea wakati klabu ikijiandaa kuelekea mkutano mkuu Juni 10 2018.
Taarifa zinasema baada ya mazungumzo, Manji amewataka baadhi ya viongozi waweze kujizulu kwanza ambao wanaenda kinyume na matakwa yake, kabla hajarejea klabuni hapo.
Manji ameomba iwe hivyo kutokana na baadhi ya viongozi ambao inaelezwa hajawataja majina kutaka waondoke kwanza ndipo aweze kurudi.
Mwenyekiti huyo wa zamani inaelezwa amefunguka kwa kusema viongozi hao anaotaka waondoke wamekuwa wakipinga uwekezaji pamoja na uwepo wake ndani ya Yanga huku akisema hafurahii namna klabu ilipofikia.
Kuelekea mkutano mkuu, jana viongozi wa matawi Yanga walikutana na kujadili mambo kadhaa kuelekea mkutano huo huku wakisisitiza kuwa kauli mbiu itakuwa ni Yusuph Manji na Mabadiliko.

0 coment�rios: