Friday, 8 June 2018

YANGA WANA HOJA ZA MSINGI KUJITOA KOMBE LA KAGAME

Na Mkubwa Kambi Anyway linalowezekana leo lisingoje kesho!! Ninavyofahamu mimi, michuano yoyote inayohusisha vilabu vikubwa vilivyo chini ya Federation ya Wanachama wa Fifa, Caf ama TFF ni lazima inawekwa kwenye kalenda maalum unless otherwise ni michuano ya kirafiki!! Hata michuano ya Sportpesa msimu uliopita ilikua ni ya kihuni tu, kwakua vilabu vyetu vina njaa ya kujitakia vilikubali kushiriki bila kua na maandalizi na matokeo yake tuliyaona. Haiyumkini Kagame Cup ni michuano inayotambulika katika ukanda wetu wa East Africa lakini nachelea kusema kwa sasa inazidiwa umaarufu hata na ile ya Ndondo Cup, sababu tu kwa sasa inaonekana haina mwenyewe kabisa!! Ni mpiga hela mmoja tu kutoka nchi jirani huamua kuketi na wapiga hela wenziwe kwenye ukanda huu na kutafuta pesa zaidi kunufaisha matumbo yao. Bahati mbaya sana hata Azam nao wanakubali kuingia kwenye mtego huu ambao hata "Ninga" hauwezi kumnasa!! Michuano hii huko nyuma ilikua na hadhi kubwa hali iliyopelekea Rais Kagame kuingiza pesa zake ambapo hutoa zawadi kwa Washindi na kupelekea michuano hiyo kuitwa "Kagame Cup" badala East & Central Africa Confederation Cup. Michuano hii hapo nyuma ilikua ikifanyika mwezi January kabla ya baadhi yako nchi kubadiki kalenda zake za ligi. Hivyo basi huko nyuma kila mdau wa soka alikua akijua ikifika January kuna "Mbungi" aidha Tanzania, Kenya ama Uganda. Sasa hivi ni kinyume kabisa, michuano hii hata haijulikani itafamyika wakati gani, kama naongopa nendeni mkaangalie ratiba ya TFF ya michuano ya mwaka huu kama Kagame Cup ilikuwepo!! Hii imepelekea hatari vilabu kushindwa kuiweka kwenye ratiba zao matokeo yake ndio haya tuyaonayo sasa!! Mara ya mwisho kufanyika nadhani ni miaka mitatu nyuma, wakati Yanga ikiwa vyema ndani na nje ya uwanja haikuwahi kufanyika!! Nani awajibike kwenye hili?! Wakati ratiba inatoka siku mbili nyuma nilijua tu michuano hii tayari imeshaingia dosari. Tanzania Bara ina wawakilishi watatu, michuano ina makundi matatu, kulikua na haja gani ya kuziweka timu mbili kwenye kundi umoja!! Tena basi ni ukweli usiofichika michuano hiyo imeletwa hapa Tanzania sababu ya timu hizo!! Hili la Yanga kujitoa kwenye michuano hiyo si geni kwani walishawahi kutoingiza timu uwanjani dhidi ya mahasimu wao Simba Sports Club! wakafungiwa wasishiriki kwa misimu mitatu, ajabu ni kwamba hata misimu miwili haikutimia wakafutiwa adhabu!! Utawafungiaje wenye mashindano yao!! Safari hii wamejitoa tena, wanazo sababu nyingi tu za msingi achilia mbali zile walizoziainisha!! Wangeweza kusema tu, michuano hiyo haipo kwenye Kalenda ya TFF ama la wangeweza kusema hatukushirikishwa kwenye maandalizi ya awali ikiwemo kupanga ratiba na mengineyo, kama walishirikishwa na wakashiriki mpaka upangaji wa ratiba basi ndugu yangu Dismas Ten aje hapa awaombe radhi WanaYanga. Nina maswali mengi kweli huwa najiuliza sipati majibu?! Hivi Cecafa inawajibika kwa nani? Katiba ya Cecafa inapatikana wapi wadau tuipitie? Viongozi wake wanapatikanaje? Na ukomo wa uongozi wao ni muda gani? Tangu nimsikie Musonye kuwa ni Katibu wa Cecafa ni umri wa mwanangu Faisal ambaye mwakani tu wallet yake inaweza kuongezeka kitambilisho cha Uraia na Kadi ya kupigia kura!! Achilia mbali jina lake kuwemo kwenye yale Madaftari yanayoandika "Mgeni anatoka Dar es salaam anakwenda Dar es salaam"!! Hata kama sababu za kujitoa kwa Yanga hazina msingi kwa waonavyo wao, ninawaunga mkono kwa asilimia 100%. Kama Musonye angekuwa raia wa Tanzania naye ilipaswa awemo kwenye kuta za Sega Dance!! Wasalam

0 coment�rios: