DONDOO 20 ZA KUJENGA NDOA YENU
1. Kuaminiana, kuungana mkono, kusaidiana na kuwa na mtazamo chanya juu ya mwenzako.
2. daima mridhie mwenza wako na umfanye ahisi kuwa ni mtu maalum.
3. Kuwa mcheshi, mburudishaji, kuwa wa maana na mwenye heshima kwa mwenzako.
4. Kamwe usifukue makaburi ya makosa yenu ya zamani. Fikiria kuhusu leo, usiendelee kulilia yaliyopita.
5. Mhamasishe na umpe matumaini mwenza wako.
6. Usimlinganishe mwenzako na watu wengine hata kwa vitu vidogo.
7. Mshangaze mwenza wako kwa mambo mapya.
8. Pendeleeni kukaa pamoja kadiri inavyowezekana.
9. Daima jiandae kwa ajili ya mwenza wako na uwe na muonekano maridadi kwa ajili yake.
10. Msikilize mwenzako, usimkatishe anapoongea. Heshima bora kabisa kwa mwenzako ni kumsikiliza anapoongea, hata kama jambo analoongea hukubaliani nalo, MSIKILIZE.
11. Epukeni kupigana, kupuuzana, kuongopeana na kukasirikiana.
12. Kuwa muwazi na umweleze mwenza wako wasiwasi na hofu yako kwa njia nzuri. Kumbuka: UKWELI HAUSEMWI VYOVYOTE WALA HAUSEMWI POPOTE.
13. Kama mwenzako amekasirika, wewe kaa kimya angalau kwa sekunde 30.
14. Epuka mabishano. Sema “kumradhi” hata kama kosa sio lako. Nusu shari ni bora kuliko shari kamili, na usalama wa ndoa yako ni bora kuliko ushindani unaoutaka.
15. Daima iombee ndoa yako iwe imara na uhusiano wenu uwe madhubuti.
16. Daima uwe mwenye shukrani kwa mwenza wako.
17. Mwambie mwenzako “Nakupenda”. neno lisikosekane katika ndoa yenu.
18. Kuwa muelewa kwa mwenza wako.
19. Hakikisheni macho yenu yanawasiliana mnapozungumza na kuongea.
20. Tengenezeni mazoea ya kula pamoja, kukaa pamoja na kusali pamoja.
0 coment�rios: