Friday, 8 September 2017

Madaktari watoa meno 7 kutoka kwa mtoto wa mwezi mmoja India

Madaktari kwenye hospitali moja iliyo jimbo la magharibi mwa Inida ya Gujarat wamefanikiwa kutoa meno saba kutoka kwa mtoto wa mwezi mmoja. "Kwa sasa mtoto yuko sawa," daktari ambaye alifanya upasuaji huo Meet Ramatri alisema. Alisema kuwa upasuiji huo ulifanya kwa njia mbili. Kwanza walitoa meno manne, na baadaye matatu. Baada ya kumfanyia uchunguzi dakari aligundua nyama nyeupe na kumtuma kwa daktari Ramatri. "Sasa mtoto huyo anaweza kunyonya," dakatari alisema, lakini aliongeza kuwa ni vigumu kujua ikiwa upasuaji huo utatatiza ukuaji wa meno ya mtoto huyo siku za usoni

0 coment�rios: