Kifo
Aliyekuwa kocha msaidizi wa timu ya soka ya Rayon Sports nchini Rwanda, Hamad Ndikumana Katauti amefariki dunia ghafla leo hii.
Chanzo cha kifo chake mpaka sasa hakijajulikana.
Ndikumana ambaye amewahi kucheza soka Tanzania akiwa na klabu ya Stand United, amewahi kuwa mume wa muigizaji Irene Uwoya na wana mtoto mmoja.
Pole kwa familia yake! Na Mwenyezi Mungu amuweke mahala pem peponi.

0 coment�rios: