Sunday, 26 November 2017

Mkomola atua yanga

Klabu ya Yanga imedhamiri kuunda upya kikosi chake kwa kusajili wachezaji vijana watakaoinufaisha klabu hiyo kwa miaka mingi. Kwa sasa kikosi cha Yanga kimesheheni wachezaji vijana wengi na kinaendelea na program ya kuwasajili wengine. Taarifa za uhakika ni kwamba Yanga tayari imemalizana na mshambuliaji wa Serengeti Boys, Yohana Mkomola ambaye anatarajiwa kuanza kuitumikia Yanga kwenye mzunguuko wa pili ligi kuu ya Vodacom Mkomola aling'ara na kikosi hicho ya timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys kilichoshiriki fainali za AFCON kwa vijana nchini Gabon mapema mwaka huu. Mwezi Agosti 2017 alifuzu majaribio kwenye klabu ya Etoile Du Sahel ya Tunisia lakini alishindwa kusajiliwa kwa kuwa umri wake ulikuwa chini ya miaka 18. Etoile walimchukua kwenye Academy yao wakiwa na lengo la kumsajili wakati atakapotimiza umri. Mkomola ataungana na wachezaji wengine waliosajiliwa na Yanga kutoka Serengeti Boyz, mlinda lango Ramadhani Kabwili na winga Said Mussa. Baada ya kutwaa ubingwa kwa misimu mitatu mfululizo, msimu huu chini ya kocha George Lwandamina Yanga inasuka upya kikosi chake. Mwishoni mwa msimu huenda ikaachana na wachezaji wengi ambao umri umewatupa mkono huku wale wa kigeni ambao wamekuwa majeruhi kwa muda mrefu wakiwa hatarini zaidi kuonyeshwa mlango wa kutokea

0 coment�rios: