Yanga yashusha kifaa
KAMA mpaka dakika hii unavyosoma hapa, Donald Ngoma, atakuwa hajatua kwenye ardhi ya Dar es Salaam, basi biashara yake na Yanga imekwisha.
Yanga ilikuwa imempa Ngoma mpaka jana Ijumaa usiku awe amerudi kazini akitokea kwao Zimbabwe alikosema anaenda kutibiwa ingawa hawana uhakika kwani aligoma kuwapa vithibitisho.
Lakini Mwanaspoti limeibua habari mpya kutoka ndani ya Kamati ya Usajili kwamba imenasa vifaa vipya viwili na kimoja kitachukua nafasi ya Ngoma ambaye kwa hali ilivyo uwezekano wa kupigwa chini ni mkubwa.
Mabosi wa Yanga wamepewa majina mawili ya mastraika wanaotakiwa kuja kufanyiwa mchujo wa mwisho akiwemo Mguinea, Bensua Da Silva ambaye ana nafasi kubwa ya kusajiliwa kwani wakala wake anasifika kwa kumiliki wachezaji wa maana.
Ingawa uongozi wa Yanga haujaweka wazi, lakini Mwanaspoti kupitia vyanzo vyake inafahamu kwamba Da Silva kuna uwezekano akasaini, pia kuna Mnigeria atakayekuja wiki ijayo kwa majaribio.
Da Silva ambaye ni mshambuliaji namba moja, inaelezwa kwamba ni mjuzi wa kufunga kwa miguu yote na hata vichwa na anatokea klabu moja ya Togo, lakini vilevile ameitolea nje African Sport ya Ivory Coast.
Katika ripoti yake ya usajili, kocha George Lwandamina, amewataka mabosi wa timu hiyo kuhakikisha anatafutwa mshambuliaji kiongozi kutokana na kikosi chake kujaa viungo washambuliaji (namba 10) akiwa na Ibrahim Ajibu, Obrey Chirwa na Ngoma huku Amissi Tambwe pekee akibaki kuwa mshambuliaji namba moja.

0 coment�rios: