Wednesday, 15 November 2017

ulimwengu wa soka Tz

Beki wa Real Madrid Dani Carvajal huenda akarejea kwenye mechi dhidi ya Atletico Madrid siku ya Jumamosi, wiki sita baada ya kupata tatizo ambalo alihisi linaweza kumaliza maisha yake ya soka. Carvajal, 25, alifanyiwa uchunguzi na kukutwa na maambukizi ya viral pericardium mwezi Septemba na hakucheza kandanda tangu siku hiyo . Aliongea na jarida la michezo la nchini Hispania , Diario Madridista (h/t AS) na amekiri kwamba taarifa za awali zilimfanya aamini kwamba soka kwake yeye ndio mwisho. " Unaanza kufikiria kwamba ni tatizo kubwa, na huenda ikawa tatizo ambalo ni sugu na kulazimika kuacha kucheza soka , hasa ukizingatia kwamba kulikuwa na matatizo kama hayo hapo awali kwa watu wengine . Lakini kwa kipindi chote hiko Madaktari waliniambia nisiwe na wasiwasi . Ni tatizo ambalo la kawaida na natakiwa kutulia tu." Iliarifiwa kwamba Carvajal huenda angerejea mapema zaidi lakini ukweli ni kwamba taarifa hizo hazikuwa sahihi , hata hivyo kocha wake Zinedine Zidane ameelezea furaha yake kuhusu urejeo wa beki wake wa kulia. Na alipoulizwa kuhusu hali yake ya sasa kuelekea mechi dhidi ya Atletico , Carvajal amesema," Kimsingi, nimeruhusiwa kucheza kutoka kwa Madaktari, kwahiyo siwezi kuwa na matatizo yoyote."

0 coment�rios: