Wednesday, 15 November 2017

ulimwengu wa soka Tz

Manchester United wanakabiliwa na changamoto kubwa sana ya kumbakiza Marouane Fellaini klabuni. United wamekuwa kwenye mazungumzo ya mkataba mpya na kiungo huyo wa kimataifa wa Ubeligiji huku Jose Mourinho akionyesha nia ya dhati ya kubaki na Fellaini Old Trafford. Fellaini ambaye anafikisha umri wa miaka 30 wiki ijayo , alipewa ofa ya mkataba mpya mwezi Septemba lakini alikataa dili hilo . United bado wamebaki na Matumaini kwamba watafikia makubaliano na Fellaini. Mkataba wa sasa wa Fellaini unafikia tamati mwishoni mwa msimu huu na pia anaweza kufanya mazungumzo ya mkataba wa awali na vilabu vya nje ya Uingereza mwezi Januari. Imearifiwa kwamba Man United hawana mpango wa kumuuza Fellaini mwezi Januari licha ya mustakabali wa mkataba wake na wapo tayari hata kumruhusu kuondoka bure mwishoni mwa msimu kuliko kumuuza januari . Mwezi uliopita Mourinho alisema kwamba ana "wasiwasi " kuhusu swala la mkataba wa Fellaini.

0 coment�rios: