Friday, 24 November 2017

Zanzibar Heroes waendelea kujifua

Katibu Mkuu wa chama cha Soka Visiwani Zanzibar upande wa Unguja Mohamed Ally Hilal amesema timu ya Taifa ya Zanzibar 'Zanzibar Heroes' inaendelea vizuri na maandalizi yake kuelekea michuano ya vyama vya Soka ukanda wa Afrika Mashariki na Kati CECAFA licha ya changamoto ya pesa inayowakabili. Akizungumza na futaa.co.tz Hilal amesema walipanga maandalizi ya wiki moja kulingana na bajeti yao lakini sasa wanalazimika kujinyima baadhi ya vitu ili kukidhi hali hiyo. Hata hivyo ameahidi kushangaza wengi katika michuano hiyo itakayofanyika Kenya mwezi ujao kwa kupata matokeo mazuri. Ufinyu wa bajeti -Tulipanga bajeti ya kufanya mazoezi ya wiki moja lakini kwa bahati mbaya mashindano yakasongezwa mbele tumeadhirika kwa baadhi kiuchumi, kwa maandalizi haikuwa tatizo kwa sababu imetupa fursa kupata muda zaidi kufanya mazoezi pamoja ili kuhakikisha tunapata matokeo, Hilal amesema. Aidha Hilal amesema ni neema kwao kwa kuwa wachezaji wamekuwa waelewa na kukubali kufanya kazi katika mazingira hayo na kukubali kujitolea bila hata kupata mshahara ama marupurupu. -Uzuri wa wachezaji wetu ni wazalendo wamekubali hali ilivyo timu yetu haina maposho ama mishahara tunajitahidi sisi kuwapa mahitaji ya kila Suki ambayo binadamu anafaa kuyapata tumejitahidi tumewaweka kambini muda mrefu tunawapa mahitaji yote lakini kwa uzalendo wao wamekubali hali hiyo" amesema Hilal. Kuhusu utayari wao kuelekea michuano hiyo Hilal amesema watategemea juhudi za kocha na wachezaji kufanya vizuri. Upinzani -Tunaamini michezo itakuwa migumu timu ambazo tutakuwa nazo zote ukiangalia ziko juu kwa hivyo tunachokitegemea kwa ushindi ni juhudi za mwalimu na uzalendo wa wachezaji ndio zitakazotuvusha tuweze kufika hatua ya nusu fainali na kuchukua ubingwa naamini kwa vijana tulio nao tunaweza tukafanya maajabu dunia ikatushangaa", ameongeza Hilal. Zanzibar Heroes wamepangwa kundi A pamoja na majirani wao Timu ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars', Rwanda, Libya na wenyeji Kenya katika michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Disemba 3 hadi 17 nchini Kenya. Tanzania CECAFA Senior Challenge Cup Kilimanjaro Stars Zanzibar Heroes

0 coment�rios: