Thursday, 21 December 2017

MBARAKA YUSUPH AENDA KUTIBIWA AFRIKA KUSINI

Mshambuliaji wa Azam FC, Mbaraka Yusuph, ameondoka nchini kuelekea jijini Cape Town, Afrika Kusini kwa matibabu ya goti lake la mguu wa kushoto. Katika safari hiyo Yusuph ameambatana makamu mwenyekiti wa Azam FC, Abdulkareem Amin 'Popat', ambaye ndiye atashughulikia taratibu zake zote za matibabu akiwa nchini humo. Baada ya kuwasili, mshambuliaji huyo kesho Ijumaa asubuhi anatarajia kuonana na daktari wa Hospitali ya Vincent Pallotti iliyopo jijini Cape Town. Yusuph alipata majeraha hayo akiwa na timu ya Taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ wakati ikicheza na Libya kwenye mchezo wa michuano ya Kombe la Chalenji ulifanyika nchini Kenya Desemba 3 mwaka huu.

0 coment�rios: