Wednesday, 28 February 2018

MAKOCHA WATATU WATAJWA NA MMOJA KUINOA ITALIA.

-Rasmi Chama cha Soka Nchini Italia FIGC kimetangaza Makocha watatu na mmoja wao kuchukua mikoba ya kuinoa timu ya Taifa ya Italia "Azzurri" . -Akiongea na waandishi wa habari Leo makamu wa raisi wa chama cha soka nchini italia Alessandro Costacurta wamefikia kuwataja Makocha watatu Antonio Conte,Roberto Mancini na Luigi Di Biagio na Mmoja wao atateuliwa kuinoa timu yao ya Taifa ya Italia. -"Tatamtangaza kocha mpya mwezi June na hatokuwa Mwingine kati ya Di Biagio,Mancini au Conte" "Kwa ujumla Mimi Kama Mimi nampendekeza Conte alishafanya kazi kubwa katika timu yetu ya Taifa hakika Alifanya vema Sana". Aliongea beki huyo wa Zamani wa AC Milan na Sasa ni Makamu wa raisi wa Chama cha Soka Italia Alessandro Costacurta. -Italia ilimtimua kazi Gian Piero Ventura mwezi November mwaka Jana baada ya kupigwa na Sweden Katika harakati za kufuzu kucheza kombe la Dunia. -Kiungo wa Zamani wa Roma na Inter Milan Luigi Di Biagio ambae kwa Sasa ni Kocha wa timu ya Taifa ya Italia chini ya Miaka 21 anatajwa kupandishwa kukinoa kikosi cha Italia " Azzurri" pia Kocha mkuu wa Chelsea Antonio Conte nae anatajwa pia Roberto Mancini nae anatajwa kuchukua mikoba ya kuinoa Azzurri.

0 coment�rios: