Tuesday, 27 February 2018

Mchambuzi maarufu KANAKAMFUMU afungiwa kujihusisha na soka

Baada ya kupigwa rugu na tff kutojihusha na soka kwa mda wa miaka mitano JOSEPH KANAKAMFUMU naye atoa neno Kanakamfumu Yaah aah nimeipokea email mida hii lakini kama nilivyowaeleza kwenye hiyo kamati ya maadili! Siku ya mchezo huo Mimi nilikuwa ndio kwanza Coach ndani ya siku kama tano hivi! Sikuwa kiongozi Mratibu na hizo leseni zilikaguliwa na Match Commissioner na waamuzi, na inaonekana kulikuwa na leseni zinafanana namba huo muda wa kung` amua hilo ningepata wapi! Uratibu wangu ulianza tar 12 Nov. 2017 hivyo hao viongozi waliopita ndio wangeweza kueleza kwa undani hilo swala! Niliomba kwenye kamati wanionyeshe hiyo kadi fake hawakunionyesha. Hata hivyo soka kwangu kama Coach sijaitendea haki sana na nilisimama kufundisha soka LA ushindani toka 2012 hivyo naishi kwa utaratubu mwingine, labda kwa kutoa maoni kama hivi Comment labda ndio mchango wangu mkubwa! Ingawa najivunia mchango Mkubwa nilioutoa kuanzia 2003 - 2006 nilipokuwa Makongo Sekondari na kutengeneza kikosi cha vijana waliokuja kuwa msaada kwenye timu ya Taifa na vilabu vingi nchini! Akina Salehe Tendega (Gk), Juma Abdul, Juma Jabu, Salum Telela, Henry Joseph Shindika, Said Ahmad ( Ortega), Jumanne Ramadhani, Abdulharim Humud, Jerry Tegete, Kigg Makasi na wengineo

0 coment�rios: