Thursday, 22 February 2018

" Mourinho ni Rafiki yangu "

Winga wa klabu ya Chelsea, Willian anajiandaa kukabiliana na 'Rafiki' yake Jose Mourinho pindi Chelsea watakaposafiri kucheza dhidi ya Manchester United katika dimba la Old Trafford siku ya Jumapili. Mourinho alimsajili Willian kutoka Anzhi Makhachkala Agosti ya 2013 na Mbrazil huyo aliwahi kuhusishwa sana na kuhamia Manchester United kuungana na bosi wake wa zamani. Lakini kuelekea mechi ya Jumapili dhidi ya United, Willian yeye anafikiria kuhusu mechi tu ambapo vilabu hivyo viwili vinapigania kumaliza nafasi nne za juu za Ligi kuu ya Soka ya Uingereza. " Ni rafiki yangu, nilikuwa na muda mzuri sana na yeye, lakini nipo Chelsea na yeye yupo Manchester United " - Amesema Willian. Chelsea wanaelekea katika mechi hiyo baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Barcelona katika mechi ya UEFA ambapo walionyesha nidhamu kubwa ya kimbinu. Huku kukiwa na safari ya kuelekea kuwakabili vinara wa EPL Manchester City na Barcelona zikiwa mechi zao za ugenini baada ya mechi ya United, winga huyo anahitaji kiwango kama walichokionyesha katikati ya wiki klabu ya Chelsea. " Ni mechi ngumu sana. Na ni tofauti kabisa kucheza mechi za ligi na za UEFA. Nafikiri tunaweza kubaki katika daraja hili na kwenda Old Trafford Jumapili na kucheza mechi nyingine nzuri ." " Inabidi tucheze vile vile dhidi ya Manchester United, nafikiri tutafanya kazi nzuri." " Dhidi ya Manchester City, nafikiri itakuwa kama dhidi ya Barcelona - wanapenda kumiliki mpira. Inabidi tuzuie vizuri na kutumia mbinu sawa na zile tulizotumia dhidi ya Barcelona. Tunaweza kushinda hizi mechi. Tutaenda kule na kujaribu kushinda."Credit #UlimwenguwasokaTz

0 coment�rios: