Mourinho atetea mbinu Vs Sevilla.
Jose Mourinho mwenye hasira ametetea mbinu zake alizotumia kwenye mechi dhidi ya Sevilla hatua ya 16 bora ya ligi ya mabingwa Ulaya ambayo iliisha kwa sare ya 0-0
Kikosi cha Mourinho kilipiga mipira 6 kwenda goli dhidi ya 25 waliyopiga Sevilla , licha ya kwamba mipira mingi waliyopiga Sevilla ilikuwa nje ya boksi ambayo haikumsumbua De Gea.
Lakini pindi alipoulizwa kwamba Alexis Sanchez ni aina ya mchezaji anapenda kucheza kwa kufuata maelekezo ya kimbinu kuliko kupewa jukumu la kucheza huru uwanjani , Mourinho alionekana kuchukizwa na swali lile,na alijibu kwa kutetea mbinu zake dhidi ya Sevilla.
" Nafikiri nyie wote au baadhi yenu mpo kwenye mchezo mpya. Uingereza kuna baadhi ya watu wanasema kwamba mawinga hawatakiwi kuzuia "
" Pindi nikikutana na David Beckham, nitamuuliza : David pindi ulipokuwa unacheza winga ya kulia Manchester United, beki wa kushoto wa timu pinzani akishambulia, ulikuwa unasimama unaangalia jukwaani ? au unarudi nyuma kumzuia ? Nitamuuliza hilo swali David ."
" Na kila mtu anajua kwamba mimi sio rafiki mkubwa wa Roy Keane au Paul Scholes, lakini nitawauliza : ' Pindi timu zenu zilipokuwa zikipoteza mpira, mlikuwa mnarejea nyuma ? au mlikuwa mnatembea uwanjani.? "
" Kwasababu sasa hivi inaonekana kwamba wachezaji wote wazuri wanatakiwa kucheza huru na pindi timu ikiwa na mpira, kitu ambacho nafikiri ni cha kipumbavu kusema . pindi timu inapokuwa na mpira , mnashambulia,na pindi timu inapokuwa haina mpira, mnazuia ."
" Rahisi kama hivyo tu.Lakini sasa hivi inaonekana kwamba kuna baadhi ya watu wanatengeneza mchezo mpya. Lakini bado sioni hiyo, kwasababu timu zinazotwaa mataji , timu kubwa Duniani sasa hivi, sio miaka 10 iliyopita , 20 au 30 , timu kubwa Duniani, sasa hivi kila mtu anajituma kufanya kazi. kila mtu anatakiwa kuwa na nidhamu ya kimbinu."Credit #UlimwenguwasokaTz
0 coment�rios: