Thursday, 22 February 2018

UJUMBE WA CHAMBUA KWA VIJANA WA YANGA SC.

Tunawapongeza vijana kwa kufuzu dhidi ya St Luis ya kule Syshells jana, ila kwa upande wa pili mnabidi mbadilike na kuongeza uwajibikaji wa kiufundi na ubunifu mnapokuwa uwanjani, kwakuwa huko tuendako patakuwa pagumu. Timu bado haijacheza katika kiwango cha kuridhisha kututia matumaini ya kufanya vizuri huko mbele, kila mchezaji aongeze bidii, lakini Mwalimu nae ana sehemu yake kwa ajili ya kuiongezea timu marifa zaidi ya ushindani wenye tija, lazima mjue kubadilika pale ambapo timu haiendi vizuri, nyie ni jukumu lenu maana ndiyo mliopo kwa sasa. Sumbueni akili zenu kila siku kwa ajili ya timu (Yanga) kila mtu aimarishe uwezo wake na aulinde, kikubwa ni kwamba lazima mjue kwamba kila mchezaji ni muhimu kujifunza kila mchezo anaocheza ili kumpa uwezo wa kujifanyia tathmini yeye mwenyewe. Nawatakia kila la kheri wachezaji wetu, mko kwenye Club kubwa yenye heshima barani Africa, jivunieni kuwepo hapo! Sekilojo Johnson Chambua Mchezaji gwiji wa zamani Yanga SC.

0 coment�rios: