Tuesday, 27 February 2018

WARUNDI KUAMUA DAR,WAMOROCCO KUAMUA BOTSWANA.

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limewataja waamuzi kutoka Burundi kuchezesha Mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga SC ya Tanzania dhidi ya Township Rollers ya Burundi utakaofanyika March 6,2018 Katika Uwanja wa Taifa DSM Saa 16.30. Mwamuzi wa kati atakuwa Pacifique Ndabihawenimana akisaidiwa na Mwamuzi Msaidizi namba moja Willy Habimana,Mwamuzi Msaidizi namba mbili ni Pascal Ndimunzigo na kamishina wa Mchezo huo atatoka Swaziland Mangaluso Jabulani Langwenya. Mechi ya Marudiano itachezwa March 16 huko Botswana na kuchezeshwa na waamuzi kutoka Morocco. Mwamuzi wa kati atakuwa Redouane Jiyed akisaidiwa na Mwamuzi Msaidizi namba moja Youssef Mabrouk,huku Mwamuzi Msaidizi namba mbili ni Hicham Ait Abou,Mwamuzi wa Akiba ni Samir Guezzaz na kamishina wa Mchezo huo atatoka Afrika Kusini ambae ni Gay Makoena. Yanga SC imefuzu hatua hii baada ya kuifunga St.Louis ya Shelisheli kwa jumla ya Magoli 2 kwa 1,huku Township Rollers ikifuzu hatua hii kwa kuwafunga El Merrikh ya Sudan kwa jumla ya Magoli 4 kwa 2.

0 coment�rios: