Wakati serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Shirikisho la Soka nchini TFF kuwasihi waandishi wa habari kuliacha suala la Zanzibar katika kipindi hiki cha Mkutano mkuu wa Shirikisho la Soka Duniani FIFA ambao utafanyika Jijini Dar es Salaam keshokutwa, Mnadhimu wa chama cha wananchi CUF Ally Saleh Alberto ameibuka na kuhoji msisistizo huo ili hali upande wa visiwa hivyo una haki ya kutambua mustakabali wa kupata uanachama ndani ya CAF na FIFA.
Ally Saleh ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Malindi, ameibuka na madai hayo baada ya kuitisha mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mapema hii leo Jijini Dar es Salaam, ambapo amesema pamoja na waandishi wa habari kutakiwa wasiulize lolote kuhusu Zanzibar, bado wao kama wawakilishi wa Wananchi wanaona kuna umuhimu wa suala hilo likafikishwa kwa Rais wa FIFA ambaye atahudhuria Mkutano wa keshokutwa.
Ally Saleh amesema lengo kubwa kwa sasa ni kutaka kuhakikisha mamlaka za Soka za Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar zinakua na mipaka yake na kutambuliwa kwa mipaka ambayo itawawezesha kufanya kazi kwa maslahi ya kila upande wa Muungano wa Tanzania.
Amesema kwa sasa kinachoendelea ni kama unyonyaji dhidi ya upande wa Zanzibar jambo ambalo limekua likijidhihirisha wazi hasa zinapoitwa Timu za Taifa pamoja na maamuzi ya wapi Timu hizo zikacheze zinapokua kwenye Michuano ya Kimataifa.
.
"Tumemuandikia Barua Rais wa FIFA kama itabahatika kumfikia na mambo tuliyo muandikia na kumfafanulia ni TFF haiwakilishi Maslahi ya Zanzibar,Mamlaka ya TFF hayajawahi wala hayafiki Zanzibar,Muundo wa TFF ni kuwa ni Vyama vya Mikoa wakati SFA inamikoa yake,TFF haijawahi kuwa na Sera ya Maendeleo inayoihusisha Zanzibar pia hakuna Kikao chochote cha Kikatiba baina ya TFF na ZFA"amesema Ally Saleh
ZANZIBAR YATAKA HAKI YA KUPEWA UANACHAMA WAO NDANI YA CAF NA FIFA

0 coment�rios: