
Mkwasa ataka Mbeya city waadhibiwe
Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga, Charles Boniface Mkwasa, amelitaka Shirikisho la Mpira wa Miguu kuichukua hatua za kinidhamu Mbeya City FC baada ya mashabiki wake kufanya vurugu katika mchezo wa ligi dhidi ya Yanga.
Yanga ilikutana na Mbeya City Jumapili ya Aprili 22 kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya na mechi hiyo ilimalizika kwa kwenda sare ya bao 1-1.
Mchezo ulisimama kwa takribani dakika 4 kipindi cha pili baada ya mashabiki wa Mbeya City kuanzisha vurugu na kufikia hatua ya kurusha mawe Uwanjani, kitu ambacho kilisababisha mchezo kutoendelea kwa muda na askari wakaingilia kati.
Kutokana na tukio hilo, Mkwasa ameomba timu hiyo vema ikachukuliwa hatua baada ya sekeseke hilo kutokea Uwanjani siku ya mchezo.
Mbali na mashabiki kufanya fujo, Mkwasa amesema pia TFF wanapaswa kuiadhibu Mbeya City kufuatia kitendo cha wachezaji kuzidi Uwanjani ilihali mmoja alikuwa ameshatolewa nje kwa kadi nyekundu.
Tukio hilo lilimfanya Kocha Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa kuanza kubishana na Kamisaa wa mchezo alipoanza kumuuliza inakuwaje City wawe 11 badala ya 10 Uwanjani wakati mmoja ameshapewa kadi nyekundu.
Wkati Mkwasa akieleza hayo, tayari Yanga wameshakata rufaa ya malalamiko kuhusiana na mchezo huo ambayo imeshawasilishwa katika Bodi ya Ligi.

0 coment�rios: