
-Kocha msaidizi wa timu ya taifa ya DRC Congo, Mwinyi Zahera yupo nchini kukamilisha mazungumzo na uongozi wa mabingwa wa ligi kuu Tanzania Bara klabu ya Yanga ili kuchukua nafasi ya kocha George Lwandamina.
-Kocha huyo raia wa DRC Congo alikuwepo nchini kwenye kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo kilipocheza na Tanzania kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki na kupoteza kwa mabao 2-0.
-Habari kutoka Yanga zinadai kwamba wameamua kutafuta kocha mwingine baada ya kushindwa kumrejesha kocha George Lwandamini ambaye amerejea kwao kuifudisha Zesco united. Yanga wanatarajia kumalizana na kocha Zahera kabla ya kuanza mechi za makundi za Caf Confederation Cup.
-Yanga wataanza kucheza mechi za kundi D May 06 ugenini dhidi ya USM Alger ya Algeria kabla ya kurudi Tanzania kucheza na Rayor Sports ya Rwanda May 16.
0 coment�rios: