Friday, 11 May 2018

Hatimaye beki wa kati wa Yanga, Kelvin Yondani amerejea mazoezini.

Yondani ameungana na wenzake na kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Polisi Kilwa jijini Dar es Salaam. Haijaelezwa uongozi wa Yanga umemalizana vipi na Yondani lakini inaonekana mambo yanakwenda vizuri kwenye msitari. Beki huyo alizua sintofahamu baada ya kuamua kubaki timu yake ikisafiri kwenda Algeria kuivaa USM Alger katika mechi ya Kombe la Shirikisho, hatua ya makundi. Taarifa za awali zilieleza mkataba wa Yondani ulimalizika na aliwasiliana na viongozi wa klabu hiyo bila ya mafanikio hasa suala la utekelezaji hadi alipoamua kuchukua uamuzi huo

0 coment�rios: