Friday, 11 May 2018

Yangu kushusha mbadala wa Ngoma

Licha ya kueleza kuwa imeyumba kiuchumi, klabu ya Yanga ipo katika mchakato wa kushusha mshambuliaji Mtogo, Djako Arafat, kutoka Welayta Dicha SC. Taarifa za ndani ya uongozi wa Yanga zinaeleza kuwa klabu hiyo inatarajiwa kumleta mshambuliaji huyo kuja kuimarisha safu ya ushambuliaji iliyo na mapungufu. Yanga inamleta Djako kwa ajili ya kusaidia Yanga inayoshiriki mashindano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika. Ujio wa Djako unatajwa kama mbadala wa Donald Ngoma ambaye amekosekana dimbani kwa muda mrefu zaidi kutokana na kusumbuliwa na majeraha. Taarifa za ujio wa mshabuliaji huyu zimezidi kushika kasi ikiwa inajiandaa na mchezo wa pili wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda utakaopigwa Mei 16 2018.

0 coment�rios: