
Na Saleh Ally
YANGA imekwama, si vibaya kusema imekwama katika tope na inaonekana ni kama vigumu sana kukomboka na kuingia katika barabara sahihi.
Yanga haiende kwa mwendo wake, ajabu zaidi inaonekana kama mambo yanakwenda haraka sana na zaidi ni kudidimia.
Mashabiki wengi wa Yanga wamekuwa ni watu wenye jazba na wanahizi kila mtu ni msaliti kwao, sasa hawataki hata kuona timu au klabu yao inatajwa.
Siku chache zilizopita, walitamani Yanga itajwe, walitamani kuiona inazungumziwa na ikiwezekana kupewa heshima kubwa kutokana na kile unachokifanya.
Lakini sasa mambo yamekuwa tofauti, ikizungumzwa Yanga ni ukata ndicho kinachosikika sana kwa kuwa imekuwa ni timu yenye maisha mazuri kwa muda mrefu, tokea mwaka 2012.
Kama unakumbuka, baada ya Simba kuifunga Yanga kwa mabao 5-0 na kubeba ubingwa, maumivu ya Wanayanga yalikuwa ya kiwango cha juu. Ndipo aliyekuwa mfadhili alipoamua kugombea uenyekiti.
Yusuf Manji aliamua kugombea nafasi ya mwenyekiti wa klabu hiyo akisisitiza kwamba klabu hiyo ilihitaji mtu imara ambaye angeweza kusimama imara na kurejesha umoja wa Wanayanga ambao walikuwa wamesambaratika baada ya kipigo kile kikali kutoka kwa watani wao.
Kwa muda aliokaa madarakani, Manji alifanikiwa kwa asilimia mia. Aliiwezesha Yanga kuwa bingwa mara nne katika misimu mitatu, ikifanikiwa kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho hatua ya makundi. Kama hiyo haitoshi, aliiwezesha Yanga kuibana Simba kushindwa kushiriki michuano ya kimataifa kwa muda wote huo.
Manji aliibana Simba kwa kuwa Yanga ilikuwa ikichulkua nafasi hiyo na kufuatia na Azam FC. Simba ikazorota na machungu yakahamia Msimbazi ambao walikuwa wakipambana kwa kila namna kurejesha heshima yao.
Kwa Yanga sasa wametumbukia katika shimo ambalo walikuwemo Simba ambao wanaonekana wamepindua kabati na huenda wako wanaona hali hiyo inaweza ikawa ni ya siku mbili au tatu, hilo ni kosa kubwa sana.
Hali inayowatokea Yanga katika kipindi hiki haiwezi kwisha wka ramli au miujiza. Na Kama Yanga wataendelea kuamini itaisha tu kwa kudra zake muumba, basi wataendelea kutesekwa kipindi kirefu sana.
Yanga hawajaingia katika shimo hilo kwa bahati mbaya. Badala yake, suala hilo lilikuwa linakua hatua kwa hatua huku ikionekana kama ni suala ambalo haliwezi kutokea.
Mwisho limetokea na kuwa mzigo mzito kwa Yanga ambayo sasa haitakiwi kufanya kazi kwa hisia pekee, badala yake uteketezaji wa vitendo unatakiwa kwa zaidi ya asilimia mia.
Wengi wa viongozi au wadau wa Yanga ni wale waliokuwa wakipiga kelele kama akina Salum Mkemi na wajumbe wenzao kuonyesha kwamba wana mipango imara sana ambayo sasa haionekani wakati Yanga ikididimia.
Watu kama hao, wakiwemo kama Katibu wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali, sasa wameanza kuona mziki ni mkubwa na utaona wamekuwa kimya hakuna anayezungumza tena kama ilivyokuwa katika kipindi cha Manji. Kwamba anajinufaisha na klabu. Sasa hayupo na mambo ni magumu.
Yanga inaweza kujikomboa na kujitoa kwenye tope na ndilo jambo linalotakiwa kufanyika. Lakini lazima ipate kiongozi ambaye atakuwa ndiye mkuu, akubali lawama zote ili kufanya mabadiliko.
Yanga inapaswa kupata mtu aliyenuia kuing’oa ilipo, lakini lazima awe mtu asiyebabaishwa na maneno au zile lawama ziliokuwa zikitolewa kama wakati ule wa Manji.
Kuikomboa Yanga lazima awe mtu mwenye ndoto ya mafanikio ya kibiashara, mtu anayeangalia kinachoingia na kinachotoka na mwenye mipango ya muda mrefu na mfupi.
Lazima mtu huyo awe ni mwenye mapenzi ya dhati na Yanga, asiyetaka kujifaidisha binafsi kwa kuwa Yanga imeathirika kwa kiasi kikubwa na watu wengi waliotaka kujifaidisha wao na nafasi zao na si klabu.
Naweka msisitizo, Yanga inahitaji mtu mkweli asiye mwoga, mwenye mipango sahihi ya biashara na uzoefu wa uongozi ambaye atarekebisha ilipofikia, la sivyo itajikuta katika mateso ya muda mrefu sana.
Kwa mashabiki na wanachama wa Yanga, punguzeni lawama. Kuweni mnaowapa moyo wanaojaribu kufanya vizuri kwa ajili ya klabu yenu. Kama mtaendelea hivyo, basi hata wenye uwezo
0 coment�rios: