Friday, 24 November 2017

simba na yanga wananikosha kumgombania

MTOKEA BENCHI. SIMBA NA YANGA ZINAVYIONIKOSHA KUMGOMBANIA MAGULI. Dirisha la usajili kwa timu za ligi kuu Tanzania bara lilifunguliwa tarehe 15 mwezi huu kuvipa fursa vilabu vya ligi kuu kujihimarisha kuelekea mzunguko wa pili wa ligi kuu ya vodacom Tanzania bara Tangu kufunguliwa kwa dirisha dogo habari inayoonekana na kujadiliwa na wapenzi wa soka ni kuhusu tetesi za klabu kongwe nchini simba na yanga kumtaka Elias magoli taarifa hii imennifanya nicheke kicheko cha huzuni kuona vilabu vyenye mashabiki wengi vinapigana kumbo kumnsa Maguli. Suala hilo linafanya niwe na maswali mengi zaidi,hivi simba na yanga hazina watu wa kutafuta vipaji vya wachezaji mpaka zinamwania maguli, hivi Hans pope na Bin kleb wanatumia vigezo sahihi kufanya usajili . Maguli sio mgeni katika soka Tanzania , amajulikana kwa ubora wake na madhaifu yake hapo ndo najiuliza hatacheza nafasi ya nani ndani ya simba kama mavugo na bocco wanasota benchi, hatacheza nafasi ya nani yanga kama Tambwe ngoma na Matteo wanasota benchiI au ni kutaka kuonesha jeuri la fedha halafu mwishoni tulie kwamba fedha za sport pesa ni ndogo Yanga walimsajili Jama mba Robert kutoka kameruni lakini hakunesha kitu jangwani na wengine wengi simba kwa jeuri La pesa za mtu wanatembea hadi ivory coast wanamleta blagnon kwa hela ndefu lakini alifika na kuwa tangazo kwenye magazeti ili ndo soka la Tanzania vilabu kumgombea mchezaji bila kujua ana ubora gani. Wakati wengine wakisema goli maguli dhidi ya Benin ndo chachu ya kutakiwa wengine wanawabeza kwamba ni kukosa watu sahihi wa kufanya usajili na hili ndo linatafuna vilabu hivi kuasjili kwa ushabiki na vichwa vya habari vya magazeti NI muda sasa vilabu vyetu kuwa na maskauti wa kutafuta wachezaji sio muda ukifika tunaanza kumgombania Maguli na kutuletea Gyan na blagnon ukions wenge anamleta Jens rehman emirates sio kwa ushabiki ila ni kuwa na mtu sahihi wa kutafuta vipaji bora bkwetu watu ambao hawajui mpira ila NI waongeaji kwenye vyombo vya habari ndo wanafanya usajil Hivi hatujifunzi kutoka kwa Timi za afrika hasa kaskazini haziwezi kusajili mchezaji kwa kukurupuka Tp mazembe kumsajili mchezaji Nni lazima afanye majaribio pale Lubumbashi man city kumsajil Jesus ilikesha nchini brazll kutazama uwezo wake ndo maana sasa hivi ni nguzo ndani ya Etihad lucas moura na oscar kuja ulaya walitazamwa muda mrefu hapa kwetu ni kumwania mchezaji anapofunga goli moja

0 coment�rios: