Friday, 24 November 2017

Stand utd yamkataa pastory athanas

Klabu ya Soka ya Stand United 'Chama la Wana' imeamua kuachana na mshambuliaji Pastrory Athanas aliyetazamiwa kujiunga na timu hiyo katika dirisha dogo la usajili. Katibu Mkuu wa Stand United Kennedy Mwangi amesema wameamua kufikia hatua hiyo baada ya mchezaji huyo kuwa msumbufu kiasi cha kushindwa kumaliza mazungumzo ya usajili wake. Amesema kwa kuwa walikuwa wanahitaji huduma yake, waliazimia kuzungumza na Singida United ambao ambao nao wakawaomba kuzungumza na Simba lakini mchezaji mwenyewe alikuwa msumbufu. -Ana usumbufu sana nafikiri ndio maana hata Singida wameshindwa kukaa naye, tuliongea naye kama mchezaji, baadae tukaongea na Singida Utd, nao wakatupa maelekezo tuwasiliane na Simba, ambao walitupa barua ya kumuidhinisha kuja kwetu. Amesema kuwa "lakini huyo mchezaji amekuja huku anadai bado anawadai Simba, mara anasema anaomba Simba wamuachie kabisa, anaongea mambo ambayo sisi hayatuhusu, yanamuhusu yeye na Simba, amesema Mwangi. Tunatafuta mwingine. Amesema baada ya kuona jambo hilo kuwa zito ndio wamefikia maamuzi ya kuachana naye kwani muda unakwenda na wanataka kufanya mipango mingine. -Tumeona muda unazidi kwenda na tutapoteza muda kwa mtu ambaye hawezi kutusaidia, hajacheza mchezo wowote toka kuanza kwa ligi, tunaangalia wachezaji wengine ambao wanaweza kutusaidia, ameongeza Mwangi. Pastory ambaye alijiunga na Simba katikati ya msimu wa 2016/17 kwa mkataba wa miaka miwili, ameshindwa kuwika kwani mbali na kutolewa kwa mkopo kwenda Singida United lakini bado kiwango chake kimeshindwa kulishawishi benchi la ufundi. Akiwa Simba SC. Hata hivyo tangu alipojiunga na Simba SC amefunga bao moja pekee bao ambalo alilipata katika mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya 16 Bora dhidi ya Polisi Dar. Tanzania Simba SC Singida United (Tanzania premiere league) Pastory Athanas (Tanzanian/ No Team)

0 coment�rios: