Tetesi za usajili msimbazi
Ili kuhakikisha wanafanya vizuri Ligi Kuu Bara na katika ile michuano ya kimataifa Simba tayari wameanza mchakato wa kumnasa mkali wa magoli kutoka Zambia Walter Bwalya
Inaaminika Simba wanaitaji kuboresha sehemu ya ushambuliaji ili kuweza kupata magoli zaidi ya moja kwa kila mechi, hivi karibuni Simba wamekuwa wakiwatumia Bocco, Luizio na Mavugo katika safu ya ushambuliani lakini wameshindwa kuonesha kile timu inaitaji.
Ili kuhakikisha swala hilo linaisha pale mbele Simba wamepanga kumsajili mkali huyo na endapo dili likitiki basi ukame wa makombe unaweza kuisha kwa wekundu hao wa msimbazi.
Taarifa zaidi zinadai vigogo hao wamemwachia kila kitu mwenyekiti wao wa kamati ya Usajili ya klabu hiyo, Zacharia Hans.
"Unajua yule jamaa (Bwalya) kama unakumbuka misimu kadhaa tulitaka kumsajili lakini dau lake likawa kubwa sana tukamshindwa, lakini sasa tumeona tufanye kila linalowezekana tumchukue, alieza kiongozi mmoja wa Simba.
"Jukumu lote tumemwachia mpiganaji mwenzetu Poppe (Hans Poppe), ahakikishe anamalizana naye na hata dau likiwa kubwa tumekubaliana kuchangishana, lengo likiwa kufanikisha mpango huo," alisema.
"Kama unavyojua, Simba ina misimu kadhaa imeshindwa kutwaa ubingwa, ndiyo maana tunafanya kila linalowezekana kuhakikisha dhamira yetu hiyo inatimia lakini pia kufika mbali katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika inayotukabili hapo mwakani," alisema.
Unaweza jiuliza Bwalya anasajiliwa ili kuchukua nafasi ya nani pale Simba? tetsi zinadai kuwa inawezekana Laudit Mavugo akatemwa kutokana na kushindwa kuonyesha uwezo wake kama ilivyotegemewa.
Wachezaji wengine wanaotajwa kutemwa ni Method Mwanjali na sababu zikielezwa kuwa ni umri kumtupa mkono, mwingine ni Juma Luizio ambaye yeye tayari ameshaweka wazi kwamba ataiandikia klabu yake barua ya kuomba kuachwa ili atafute maisha kwingineko.
0 coment�rios: